Sisi ni kina nani

Kampuni ya uchapishaji ya Epsilon inaaminika kwa uchapishaji katika muungano wa Waafrika. Kimsingi, tunafanya kazi na mashirika na taasisi kuunda machapisho yanayosababisha athari chanya katika jamii. Kama watia saini wa makubaliano ya wachapishaji wa malengo ya maendeleo endelevu, tunajitahidi kuchapisha kazi zinazo himiza utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu, na kazi ambazo zinafahamisha, kustawisha na kuhimiza utendaji wa kazi. Tunajitahidi kutimiza hili kwa kukusaidia kuwasilisha ujumbe wako kwa ufupi na ufasaha ili kukuunganisha na hadhira lengwa na washikadau.

Kazi tunayofanya

Kama wachapishaji wa Epsilon tunaelewa kuwa mawasiliano huwa zaidi ya kusambaza ujumbe. Kwa kuchunguza kwa makini kila kipengele cha ripoti yako, tunajitahidi kuwasilisha mambo yote muhimu ya kiini cha ujumbe wako.

Umaakini wa michakato yetu unaongozwa na kujitolea kwetu kuzidisha matarajio ya hadhira yako lengwa. Tunaunda mawasiliano na ujumbe wenye ushawishi ili kuvutia hadhira lengwa.

Huduma zetu za uhariri, tafsiri, uchapishaji na uchapaji zinakusudia kuwasilisha ujumbe wenye athari katika viwango vyote vya jamii. Tunatoa huduma pana za uhariri, tafsiri, uchapishaji na uchapaji katika lugha ya Kingereza, Kiswahili na Kifaransa.

Matini

Uhariri wa kiundani
Uhariri wa muundo
Kusoma kwa prufu
Tafsiri

Picha

Picha halisi
Picha zenye ujumbe
Grafu
Michoro

Vile tunafanya kazi

  • Kila unaposoma kitu fulani ni rahisi kusahau namna ujumbe huo ulikufikia. Uchapishaji ni zaidi ya uchapaji na usambazaji wa maandishi; uchapishaji unajumuisha shughuli nyingi na juhudi. Lakini, kuwa mchapishaji kuna maana gani?

  • Watu wengi huchukulia kuwa wachapishaji ni wachapaji, ila kwa kweli, wachapishaji ndio wenye jukumu la kila kiingiacho kwa tunachokisoma na namna tunakisoma. Chapisho nzuri huja pamoja wakati ujumbe wake ueleweka akilini na wasilisho lake kuvutia moyo.

  • Ingawa awali uchapishaji ulihusisha uchapaji wa vitabu, magazeti na  majarida, taaluma hii imepanuka na kuhusisha usambazaji wa ujumbe mtandaoni. Mchapishaji ana jukumu kubwa zaidi ya lile la kuwasilisha ujumbe kwa umma.

Malengo ya maendeleo endelevu kwa wote

Kama watia saini wa makubaliano ya wachapishaji wa umoja wa mataifa, ni jukumu letu kuhakikisha kuwa ushawishi wetu unatumiwa kuboresha maisha ya binadamu. Makubaliano ya wachapishaji wa malengo ya maendeleo endelevu ya umoja wa mataifa, yanawakilisha ushirikiano wa kujitolea kujitajidi kujenga maisha bora ya baadaye katika viwanda vyote vya uchapishaji.

Nchi ambazo machapisho tumefanya yamefika

1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
1

Kenya

2

Tanzania

3

Uganda

4

Ethiopia

5

Somalia

6

Rwanda

7

Burundi

8

Zanzibar

9

Angola

10

Msumbiji

11

Afrika Kusini

12

Ushelisheli

13

Mauritius

14

Komoro

15

Ghana

16

Nigeria

17

Burkina Faso

18

Benin

19

Mauritania

20

Moroko

21

Gambia

22

Misri

23

Senegal

24

Marekani

25

Uingereza

26

Jamuhuri ya Ireland

27

Zambia

28

Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

29

Italia

Maoni ya wateja wetu

Nataka kutoe shukrani za dhati kwa kikundi chenu. Mlitufanyia kazi nzuri, mkatufaidi katika ujuzi wa kiufundi, kazi yetu ikakamilika vyema. Mlitimiza zaidi ya matarajio yetu. Asanteni!

H.D

Ningependa kushukuru kikundi chenu kwa kutufaa wakati tulihitaji msaada wenu sana. Ripoti iliwasilishwa kwa muda, ilikuwa nzuri na ilipokelewa vyema. Asante!

M.W

Nawaandikia kuwafahamisha kuwa ripoti iliwasilishwa na kupokelewa vyema. Shukrani za dhati kwa kikundi kizima cha Epsilon kwa kujitahidi kufanikisha ripoti hii. Ni kazi iliyofanywa kwa utaalamu mkubwa.

M.A

Ningependa kuwashukuru kwa kazi nzuri mliotufanyia kutoka kwa kuhariri, masimulizi ya picha hadi kwa usanifu wa picha na mengine mengi. Tunafurahia sana huduma bora mnayotupa na utaalamu mkubwa mliodhihirisha katika mchakato mzima. Kazi yenu yenye umakini nzuri ilituwakilisha vyema.

H.Y

Uanzie wapi?

Tunakusaidia kuwasilisha ujumbe wako kwa ufasaha kwa kuratibu na kupanga maudhui huku tukisimamia na kujadiliana kwa kina katika mchakato wote. Tunafanikisha hili kupitia njia na namna mbali mbali zitakazo kufanya kufikia hadhira yako na kuwahimiza kuchukua hatua mara moja.

Tunatoa huduma za ushauri wa ndani unaolenga kuunda mswada wako hadi kuwa chapisho kamili lililo na ujumbe wa kushawishi fikra. Kwa kweli umoja ni nguvu.

Tukusaidie na huduma gani??
Tuandikie barua pepe

Tunajua kuwa kuandaa chapisho sio kazi nyepesi. Kutoka kwa kuchagua cha kufanya, mpangilio, muundo na mtiririko wa mantiki ya ujumbe, hadi kwa toni na muundo wa lugha ya chapisho, tunajitahidi kuhakikisha kuwa kazi yako ina mantiki na ni faafu na inaeleweka.

© 2024 Epsilon Publishers Limited