Esther Azinga

Mhariri wa Kiswahili

Esther Azinga ana shahada ya kwanza katika elimu (Kiswahili/Dini) kutoka Chuo Kikuu cha Moi, Eldoret na Shahada ya uzamili katika usimamiaji biashara kutoka Chuo Kikuu cha Kenyatta.

Alifunza lugha ya Kiswahili na Fasihi katika shule ya upili, kwa miaka sita. Alikuwa mtahini wa Fasihi katika mitihani ya kitaifa kwenye Baraza la Mitihani ya Kitaifa la Kenya, kwa miaka 18.

Alifanya kazi ya kutafsiri na kuhariri makala na vitabu katika shirika la kidini kwa miaka 13. Ni mtaalamu wa kutafsiri na kuhariri Kiingereza/Kiswahili.  Ameshiriki katika shughuli ya kutafsiri na kuhariri vitabu vya hadithi za watoto na miongozo ya mafunzo. Ametafsiria mashirika mingi miongozo ya mafunzo na makala mengine.

Mbali na kazi yake, alihudumu kama mwenyekiti wa Bodi la Usimamizi la shule ya msingi ya St. George’s, Nairobi kwa kipindi cha miaka 3. Esther ni mhadhiri wa kozi za biashara katika chuo kikuu cha KAG EAST.