Esther Kioko

Msaidizi Mtendaji

Esther Kioko ni msimamizi wa ofisi mwenye uzoefu, ujuzi mzuri wa mawasiliano na teknolojia ya habari ambao hutoa msaada muhimu kwa ofisi ya Mkurugenzi Mkuu.

Esther ana uzoefu wa zaidi ya miaka mitano katika uendeshaji wa utawala na shughuli za ofisi. Kupewa majukumu mbalimbali kumemwezesha kutumia uwezo wake kamili kutoka kuhifadhi kumbukumbu, mipango ya kifedha, udhibiti wa mawasiliano, kubuni mifumo ya kuhifadhi kumbukumbu, kuhakikisha shughuli zote za ofisini ziko sawa , na mengi zaidi.

Anafanya jukumu muhimu katika kuhakikisha uendeshaji laini wa mfumo wa kuhifadhi kumbukumbu zote za kampuni, ukaguzi na kuidhinisha maombi ya ugavi, kushughulikia mawasiliano ya maandishi na ya kinywa ndani na nje ya ofisi, kuhakikisha vifaa vya ofisi vinahudumiwa na kudumishwa vizuri, na kuweka mazingira ya ofisi kuwa na utaratibu wakati wote.

Anazingatia uadilifu na ana msukumo wa kujitegemea; anapenda kutalii sehemu mpya na yuko tayari kujaribu uzoefu mpya.