Gacoki Kipruto

Mwanachama wa Bodi

Hamasa ya Gacoki ni kuongeza fursa za kiuchumi. Anakumbuka wakati alipokuwa mtoto tu, angekula plums hadi kushiba shambani kwa shangazi yake na bado akasikia hadithi za watu wanaokosa chakula, umbali wa takriban kilomita 200 tu.  Hili lilimfanya asome biashara na kilimo, kwa matumaini ya kuunda masoko na miundombinu itakayowezesha wakulima kufikia masoko ya mazao yao na kuhakikisha kuwa watumiaji wanaweza kupata chakula wanachohitaji.

Gacoki sasa ni mtaalamu wa maendeleo ya kimataifa ambaye uzoefu wake unajumuisha biashara ya kikanda, utawala, benki, na utafiti. Amesaidia kuunda mazingira yanayowezesha biashara kupitia mipango ya maendeleo, kuimarisha sekta mbalimbali zinazoathiri sana maendeleo na amefanya kazi na biashara na taasisi ili kuhakikisha kuwa wanazalisha athari endelevu. Katika kazi yake, anatumia zana ikiwemo utafiti, mafunzo,kufundisha, uongozi na kutoa huduma za ushauri.

Gacoki ana umilisi mkubwa katika kuzalishaa na kudumisha ushirikiano katika misingi ya wadau mbalimbali kutoka serikali hadi wazalishaji wa msingi.