Huduma zetu

Uchapishaji ni ujumuishaji wa usanifu wa picha na mchakato wa uhariri. Mchakato wa kina wa kazi yetu unahakikisha kuwa chapisho lako lina mpangilio mzuri ili kuwasilisha ujumbe ifaavyo kwa hadhira lengwa.

Mchakato wa Uhariri

  • 1

    Uhariri wa kiundani

    Uhariri wa kiundani unahusisha mapitio ya maandishi, mpangilio na uwasilishaji wa ujumbe kutoka kwa mada hadi tamati ya chapisho. Tunajitahidi kuhakikisha kuwa muundo, ujumbe, lugha, mtindo na uwasilishwaji wa chapisho ni faafu kwa hadhira lengwa.

  • 2

    Uhariri wa muundo

    Uhariri wa muundo unakusudia kutimiza usahihi, uwazi wa kuelewa na pia uthabiti wa chapisho. Ndiyo hatua inayofuata uhariri wa kiundani. Hii kwa kawaida inahusisha kukagua iwapo ujumbe ni sahihi, wazi na rahisi kueleweka. Uhariri wa muundo pia unahusisha kukagua ukweli, kwa mfano kukagua usahihi wa majina, tarehe, mifanyiko ya awali na mengine mengi.

  • 3

    Kusoma kwa prufu

    Kusoma kwa prufu ndiyo hatua ya mwisho ya mchakato wa uhariri. Hatua hii hufanyika kabla mswada haujawasilishwa kwa mchakato wa usanifu wa picha. Katika kusoma kwa prufu tunahakikisha kuwa matini haina makosa ya hijai, sarufi au yale ya uakifishaji.

  • 4

    Tafsiri

    Aghalabu, uhalisia na maana ya ujumbe huweza kupotea wakati wa tafsiri baina ya lugha husika. Tunahakikisha kuwa uhalisia wa matini chanzi unabeba ujumbe uliokusudiwa hadi kwa tafsiri ya lugha lengwa. Tunatoa huduma za tafsiri kwa lugha zilizotambuliwa kutumika na umoja wa mataifa hasa, Kingereza, Kifaransa na Kiswahili.

Huduma za ziada uhariri

  • 1

    Uundaji wa ujumbe

    Uundaji wa yaliyomo huchangia ujumbe ambao hutumiwa kwa njia mbali mbali, ambazo ni  zilizopigwa chapa na zile za kutumiwa mtandaoni. Tutakuelekeza katika kila hatua ili kuhakikisha kuwa ujumbe wako ni fasaha na unaoeleweka. Tunaunda ujumbe uliochapishwa kwa kupigwa chapa na unaotumiwa mtandaoni, kama vile ripoti, majarida, mkusanyiko wa taarifa, ujumbe wa tovuti, blogu na ule wa mitandao ya kijamii.

  • 2

    Uandishi wa nakala

    Uandishi wa nakala ni kipengele muhimu katika mchakato wa kuunda ujumbe. Bila uandishi wa nakala ujumbe utakuwa haujakamilika. Tunaunda mada za kujieleza, matini na vibonzo vya uhariri kwa uchapishaji mdogo mdogo kama vile ujumbe kuhusu kampuni, vipeperushi, magazeti na majarida. Kwa njia hii, tunajitahidi kukusaidia kukuunganisha kikamilifu na hadhira yako lengwa.

Vipengele vya usanifu wa picha

  • 1

    Picha

    Siku hizi, ukilinganisha na hapo awali, picha za hali ya juu hutumiwa kuibua ushirikiano wa kina na maandishi ili kuunda matini yenye ushawishi mkubwa. Tunatumia picha tulizochagua kwa kina na zilizo ratibiwa ili kuboresha machapisho yako mbali mbali. Wataalamu wa wa kupiga picha wanajitahidi kuandaa picha sahihi ambazo zitaongeza uzuri wa juhudi zako za kuchapisha.

  • 2

    Michoro

    Mbali na picha nzuri, michoro huweza kuwasilisha ujumbe wenye athari kubwa, na hususan hutumiwa katika mchakato wa uhariri. Michoro inaweza pia kuwasilisha hadithi katika mfumo wa katuni ya kisasa au kwa kitabu cha michoro. Ushirikiano wetu na wataalamu wa uchoraji, umetusaidia kuunda michoro iliyo na maana itakayotumika katika machapisho lako. Hili linakupa nguvu za kusimulia hadithi yenye athari ya milele.

  • 3

    Picha zenye ujumbe na grafu

    Picha zenye ujumbe hurahisisha kuelewa kwa dhana ngumu kwa kuzigawa dhana hizo katika vipengele vidogo vidogo vya ujumbe unaoeleweka. Zaidi ya hilo, pia huwezesha mpumziko wa akili kwa msomi anapopekua ripoti ya kitalaamu ambayo wakati mwingine huchosha kuisoma, na geni kwa wale ambao hawaelewi msamiati wa kitaaluma unaotumika. Matumizi yetu ya picha zenye ujumbe katika ripoti za kitaaluma yamebinafsishwa kukidhi mahitaji ya mpokeaji lengwa, ikiwemo watunga kanuni na washikadau.

Watu

Maeneo na mandhari

Miji na viwanda

Michoro inayohusu maslahi ya binadamu

Michoro ya mimea

Michoro halisi

Michoro yenye ujumbe

Michoro yenye ujumbe

Michoro yenye ujumbe

Grafu za bar na chati pau

Grafu za mstari

Grafu za utandabui

© 2024 Epsilon Publishers Limited