Karanu Muchiri

Katibu wa Bodi

Karanu Muchiri ni kiongozi anayezingatia matokeo na mwenye umahiri mkubwa katika masuala ya ushuru, uwezeshaji biashara, na uwasilishaji mkakati. Katika tajiriba yake ya kazi, amefanikiwa kuunda ushirikiano kati ya sekta mbalimbali kama vile nishati mbadala, utengenezaji vitu viwandani, na usafirishaji, kuhamasisha ufuataji sheria, kuleta ufanisi katika biashara na kugundua nafasi mpya za kiuchumi.

Uwezo wa Karanu wa kufafanua mifumo tata ya ushuru na kukuza mazungumzo yaliyo wazi kumemfanya atambuliwe kama mshauri anayeaminika kwa biashara nyingi na jamii nyingi vilevile. Miradi yake imeimarisha  ufuataji sheria na vilevile imewezesha sekta za viwanda kupitia katika mazingira ya udhibiti kwa ujasiri na uwazi.

Karanu, aliye na ujuzi wa kuwasiliana na pia mshauri, ametia fora katika kugeuza mikakati kuwa vitendo, kuwaunganisha washika dau mbalimbali, na kuimarisha timu zenye kustahimili. Uwepo wake unaleta mtazamo unaoelekezwa na suluhisho, fikra zenye ubunifu, kujitolea thabiti kusababisha thamani yenye kudumu.