Sisi ni kina nani

Sisi ni kampuni ya uchapishaji iliyo shinda tuzo. Tunaelewa kuwa mawasiliano ni zaidi ya usambazaji wa ujumbe. Tunaunda chapisho lako tangia mwanzo wake hadi ukamilisho wake, ili chapisho lako liwasiliane na hadhira lengwa ifaavyo. Kama watia saini wa Mkataba wa malengo ya maendeleo endelevu ya wachapishaji, tunajitolea kuchapisha kazi ambazo zinaeleza kwa ufasaha malengo ya maendeleo endelevu ambayo muungano au taasisi yako inajitahidi kufanikisha. Kazi ambazo tumechapisha zimesomwa katika nchi nyingi za Afrika, na ripoti hizo zimeshughulikia masuala mengi ya maendeleo ya malengo endelevu.

Kusudi letu

Kutoa usaidizi wa kiufundi kwa mashirika kupitia kuhariri, kutafsiri, ubunifu wa michoro, uchapishaji na kupiga chapa, ili kukuza uwezo wa kuathiri wa mawasiliano yao.

Maono yetu

Kuathiri hadi maili ya mwisho.

  • Kazi yetu

    Tunatoa huduma ya uhariri, tafsiri, usanifu wa muundo, uchapishaji na uchapaji ili kukusaidia kuzungumza ujumbe wako kwa hadhira yako kwa njia yenye ushawishi.

  • Mbinu yetu

    Tunafanya bidii kuhakikisha kuwa chapisho lako ni bora zaidi. Uchapishaji mzuri unamaanisha kazi ambayo inavutia umaakini kwa kuwa imewasiliana kikamilifu na hadhiria lengwa.

  • Filosofia yetu

    Tunahakikisha kwamba ujumbe wako unawasilishwa kwa njia fupi na thabiti ili uweze kutuma ujumbe unaoheshimika na wenye nguvu unaosikika na kuimarisha ujumbe wa msingi wa maandishi yako.

  • Maadili yetu

    Maadili yetu yamejikita katika kazi tufanyayo. Tunapima ubora wa kazi yetu kwa kuangazia maadili matatu yasiyobadilika: Tunafanya kazi kwa uadilifu; tunachukua jukumu la ubora wa kazi; tunawasilisha kazi nzuri.

Kusudi letu

Tunajitolea kuchapisha kazi, kimsingi kwa taasisi na miungano, kushirikiana nao ili kuwasaidia kuunda machapisho yatakayo wasiliana ujumbe wao wa kimsingi kwa washikadau wao muhimu.

Uongozi

Kufanya kazi ipasavyo ni miongoni mwa maadili yetu muhimu. Tunafanya bidii kila siku kuchapisha kazi inayoendeleza athari chanya katika jamii. Tunaweka wazi kile tunachomaanisha tusemapo kuwa tunafanya mambo ipasavyo.

© 2024 Epsilon Publishers Limited