Mumbi Gichuhi

Mkurugenzi Mkuu na Mhariri Mkuu

Mumbi Gichuhi ni mchapishaji mzoefu mwenye tajriba ya zaidi ya miaka 15. Lengo lake ni kutumia maneno yaliyoandikwa kuathiri na kukuza athari chanya ya kijamii. Ameongoza na kufanya kazi na timu mbalimbali za wahariri na usimamizi wa miradi duniani kote.

Amesimamia machapisho kadhaa yanayotumia lugha nyingi ambayo yamekuwa yakitumiwa katika nchi kadhaa za Kiafrika, na pia barani Ulaya na Marekani. Machapisho hayo yamejumuisha ripoti za kiwanda, jarida, makala na vitabu katika fani mbalimbali, ikiwa ni pamoja na utalii, uchumi, nishati na usawa wa kijinsia na mazingira.

Kinachompa kuridhika zaidi ni kwamba kupitia ripoti hizi, anaona kigezo kimoja au kingine cha athari kuu ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs), ambayo anajitolea sana kuunga mkono. Hii ni kwa sababu anamini kwamba uchapishaji ni mojawapo ya njia ya kimsingi ambayo taasisi, mashirika na kampuni zinaweza kutumia kuwasiliana mchango wao kuelekea kwa lengo hili.

Yeye ni muamini mkubwa wa nguvu za ushikamano na ushirikiano, kwa sababu anaamini kuwa mafanikio ni juhudi za pamoja kwa faida kubwa zaidi ya lengo lililokubwa kutuliko sisi. Kufikia kikomo hiki, yuko tayari kwa kazi ya ushirikiano na watu na taasisi zenye fikra kama yake.

Zaidi ya haya, amekuwa mzungumzaji mwalikwa na mshiriki katika majukwaa mbalimbali, hasa yale yanayohusu wanawake katika uongozi, kwani hili ni eneo ambalo lina umuhimu mkubwa kwake.

Anafurahia kitabu kizuri, muziki, kusafiri na sanaa.