Changieni Rasilimali
Mifano ya kurasa zilizotumiwa
Muhtasari
Kikundi cha Utendaji Kazi cha Mabadiliko ya Anga Kenya (KCCWG) ni muungano wa kitaifa wa mabadiliko ya anga unaojumuisha ofisi 270 zile za kinyumbani na zile za kimataifa zinazoangazia kushughulikia chanzo na athari ya mabadiliko ya anga Kenya, Afrika na kwingineko.
KCCWG inahusisha maeneo tisa ya mada: ukuaji wa miji, maji, misitu, nishati, biashara ya utalii na viwanda. Mradi mmoja wa KCCWG ni Changieni Rasilimali (CRM), uliotafsiriwa kama Contribution to Natural Resources kwa Kingereza, unaokusudia kuimarisha kuchukua hatua kwa mabadiliko ya anga Kenya kwa maeneo yaliyomakavu kwa kiwango cha wastani na yaliyo makavu kabisa. KCCWG na washirika wake wanakusudia kuangazia uwezo mdogo wa nchi, washirika wasiokuwa wa nchi na jamii maskini ili kuchukua hatua kwa mabadiliko ya anga kwa kuhimizi wananchi kushiriki katika hatua za kukabidhi na kuzuia mabadiliko hayo kinyumbani, kitaifa na katika viwango vya kiulimwengu.
Mradi wa CRM unalenga kuimarisha maelewano, maarifa na kutambulika kwa mabadilko ya hali ya anga kwa viwango vyote na kuimarisha mfumo wa ushirikiano kwa kutengeneza na kutekeleza kanuni za hali mbaya ya mabadiliko ya anga na sheria za kuyazuia huku Kenya. Zaidi, KCCWG inaunda uunganishi wa mabadiliko ya anga katika gatuzi ili kuhakikisha ushirika mkubwa wa shughuli za mradi kwa wananchi na wasiokuwa wananchi kwa gatuzi lengwa. Kupitia kwa viunganishi hivi KCCWG inakusudia kuhakikisha umiliki wa shughuli za miradi kwa makundi lengwa na kuunda msingi wa kusambaza ujumbe, elimu na vifaa vya mawasiliano.
Mchango wetu
Uhariri
Kuhariri kiundani
Kusoma kwa prufu
Picha
Kutafuta picha
Usanifu
Usanifu wa mtindo
Usanifu wa picha
Uchapishaji
Nakala zilizoundwa tayari kwa uchapaji
Nakala zilizopigwa chapa
Mwaka wa uchapishaji: 2012