Je Wajua?

Maswali ya Watoto kuhusu Haki Zao

Mifano ya kurasa zilizotumiwa

Muhtasari

Kitabu hiki shawishi kinatumiwa kama kifaa cha kufundishia wasichana wadogo kuelewa na kuhakikisha haki zao za kibinadamu zinatekelezwa, msisitizo ukiwa haswa kwa haki za wasichana. Kitabu hiki kinahusisha mkusanyiko wa hadithi zilizopeanwa na watoto walio na ujasiri wa kueleza matatizo ya uchungu waliopitia, huku wakipitisha ujumbe muhimu kwa rika yao.

Kwa kuwa ujumbe huu wenye uzito hauwezi kufikia kila msichana, kitabu hiki ni nuru ya mwanga kwa wasichana, kikiangaza kuelewa kwa haki zao na kuwahimiza kuzungumza wanapohisi wanakandamizwa. Zaidi, kinajibu maswali mengi yaliyoulizwa na watoto, kikipeana mwongozo kwa kuzingatia mfumo wa sera za Tanzania.

Matamanio yetu ya jumla ni kutimiza ahadi zilizopeanwa kwa watoto, kuhakikisha usalama wao na ulinzi nyumbani, shuleni na wakiwa katika jamii. Kitabu hiki kinatoa rasilimali muhimu ya kutimiza lengo hili na kuunga mkono ulinzi wa haki za watoto.

Mchango wetu

Uhariri
Kuhariri kiundani|
Kusoma kwa prufu

Kutafsiri
Kutafsiri matini kutoka Kingereza hadi Kiswahili

Michoro
Kuunda michoro ya chapisho
Usanifu wa picha

Uchapishaji
Nakala zilizoundwa tayari kwa uchapaji
Nakala zilizopigwa chapa

Mwaka wa uchapishaji: 2018

Lengo la Malengo ya Maendeleo Endelevu linalohusiana na chapisho