Mau Mau in Meru
The Untold Story
Mifano ya kurasa zilizotumiwa
Muhtasari
Kitabu hiki kinaangazia jukumu la Mau Mau kipindi cha ukoloni Kenya. Jamii ya Wakikuyu inaonwa pakubwa kama waanzilishi wa kupigania uhuru wa Afrika. Hata hivyo, matini hii inaangazia jamii ya Meru na jukumu lao katika Muungano wa Mau Mau kwa kupeana taswira ya kwanza halisi ya Mau Mau kupitia kwa jicho la Wameru.
Kitabu hiki kimeandikwa na JST Kamunchuluh na kinachanganua sababu halisi, asili na mafanikio ya Mau Mau, kuziba pengo la Historia na kutupilia mbali uongo wa Ulaya kuhusu Afrika. Kamunchuluh alilelewa gatuzi la Meru maasi. Alishuhudia hali za moja kwa moja zilizopelekea maasi, akaona uchipukaji wa viongozi wa vita vya Mau Mau Meru na chanzo, ukuaji na hali halisi ya Mau Mau.
Ndani ya kitabu hiki, anaeleza safari kutoka upinzani usio wa vurugu, vita vya Mau Mau na ufufuo wa Mau Mau na kumaliza hadithi kwa maelezo ya kimamlaka ya mahusiano kati ya Mau Mau Meru, uongozi wa Kenyatta na umma kwa jumla, ikifikia kilele cha vita vya Meru Januari 26, 1965. Matini hii ni muhimu kwa wanafunzi wote na wasomi wa historia ya ukoloni Afrika na utawala wa Mwingereza.
Mchango wetu
Uhariri
Kuhariri kiundani
Kusoma kwa prufu
Kutafuta picha
Kukusanya picha na ramani kutoka kwa Makavazi ya Kitaifa ya Kenya
Usanifu
Usanifu wa muundo
Usanifu wa picha
Uchapishaji
Nakala zilizopigwa chapa
Mwaka wa uchapishaji: 2020