Mwongozo wa BlueBiz wa Mafunzo ya Ujasiriamali

Mifano ya kurasa zilizotumiwa

Muhtasari

Mradi wa BlueBiz, unaoongozwa na TechnoServe kwa kushirikiana na Shirika la Mastercard, unashughulikia vizuizi vikuu ambavyo wanawake na wanaume hukabiliwa navyo katika kuanzisha biashara ndogo ndogo katika Uchumi Samawati wa Kenya. Ikitumia kikamilifu tajriba yake na mafunzo iliyopata kutoka kwa juhudi za biashara za vijana za awali, TechnoServe, kupitia BlueBiz, inawalenga wajasiriamali vijana 15,000 katika kaunti za pwani nchini Kenya ili kuendeleza ukuzaji wa biashara ndogo sana, ndogo na za wastani (MSME) kama njia ya kupunguza umaskini. Mradi huu unasisitiza kuendeleza ujuzi, kupata fedha, kuunganishwa na soko, na kuboresha uongozi kwa washiriki. Kwa kushirikiana na mashirika ya eneo hilo pamoja na washika dau,  TechnoServe inalenga kutumia mradi wa BlueBiz kukuza nafasi endelevu za uchumi na kuimarisha ustahimilivu wa vijana katika maeneo yaliyotengwa ambayo yanalengwa.

Mchango wetu

Kutafsiri
Kutafsiri Kiingereza kwa Kiswahili

Ubunifu
Ubunifu wa michoro wa toleo la Kiingereza na la Kiswahili la Kitabu cha Mazoezi cha Washiriki
Uchapishaji kupitia tarakilishi
Uchapishaji
PDF iliyo tayari kuchapishwa
Faili ndogo ya PDF iliyo rahisi kushiriki na watu mtandaoni

Mwaka wa uchapishaji: 2024

Lengo la Malengo ya Maendeleo Endelevu linalohusiana na chapisho