Mabango

Mifano ya mabango kutoka kwa mfululizo huu

Muhtasari

Sound of Silence ni maudhui ambayo tulijenga kuangazia udhaifu na hatari zinazowakabili hasa wasichana wadogo. Tulipewa jukumu na Equality Now kuandaa mfululizo wa mabango yatakayozungumza ujumbe ulioandikwa bila kutambulika na watoto hawa.

Mabango haya yaliwasilishwa kwa mara ya kwanza Mauritius katika mkutano wa Umoja wa Afrika wa Kamati ya Wataalam wa Kiafrika kuhusu Haki na Maendeleo ya Mtoto. Kazi hii iliwasilishwa kwa mfumo wa mabango kwa sababu ni rahisi kuyasafirisha katika nchi ambazo yaligawanywa baadaye. Nchi hizo ni pamoja na Mauritius, Kenya, Uganda, Tanzania, Gambia na Mauritania.

Mchango wetu

Mchango wetu
Dhana ya maudhui
Tumekuza dhana ya Sound of Silence, ili kuwakilisha waathirika wasiohesabika wa unyanyasaji ambao wanalazimika kukaa kimya kwa sababu ya hofu ya kulipiza kisasi, aibu, vitisho kutoka kwa wanaowadhulumu, na hata kutengwa na jamii zao.

Michoro
Tuliunda na kutengeneza michoro ili iambatane na ujumbe katika kila kipeperushi

Tafsiri
Tulitafsiri vipeperushi hivyo kutoka Kingereza hadi Kiswahili na Kifaransa kwa sababu vilipaswa kusambazwa kwote Afrika, katika nchi zote zinazozungumza Kifaransa na Kingereza.

Usanifu
Usanifu wa picha

Uchapishaji
Nakala zilizoundwa tayari kwa uchapaji
Nakala zilizopigwa chapa

Mwaka wa uchapishaji: 2017

Lengo la Malengo ya Maendeleo Endelevu linalohusiana na chapisho