Recognising Sacred Natural Sites and Territories

An Analysis of how the Kenyan Constitution, National and International Laws can support the recognition of Sacred Natural Sites and their Community Governance Systems

Mifano ya kurasa zilizotumiwa

Muhtasari

Ripoti hii inachunguza iwapo katiba ya Kenya ya 2010 na mfumo wa kisheria wa sera na taasisi nchini Kenya inatambua na kuunga mkono au kukandamiza haki na majukumu ya jamii ya kusimamia na kulinda maeneo matakatifu kiasili na  maeneo ya kimipaka kulingana na mfumo wa usimamizi wa kawaida na kutegemea kanuni zao wenyewe.

Ripoti hii ni mchango muhimu wa kuelewa katiba ya Kenya 2010 na sheria nyingine za kitaifa. Inaimarisha utambulisho na kuunga mkono ulinzi wa jamii wa maeneo matakatifu ya kiasili kulingana na mfumo wa usimamizi wao wa kawaida.

Zaidi ya hayo, inaonyesha ukuaji wa kila mara wa mifumo ya kisheria ya Kenya kuelekea kwa kutambua mihimili ya  “Sheria ya Dunia“ na kuweka mfumo wa kuunda sheria za kulainisha kabisa usimamizi wa mazingira ndani ya nchi na kwingineko. Maeneo matakatifu ya kiasili ni matukio muhimu ya kimazingira, kitamaduni na pia ya kiimani duniani ambayo ulinzi na heshima yake na jamii husika ni lazima  kwa afya na ustawi wa kizazi cha sasa na cha baadaye.

Mchango wetu

Uhariri
Kuhariri kiundani
Kusoma kwa prufu

Uchapishaji
Nakala zilizoundwa tayari kwa uchapaji
Nakala zilizopigwa chapa

Mwaka wa uchapishaji: 2013

Lengo la Malengo ya Maendeleo Endelevu linalohusiana na chapisho