Uwasilishaji wa michoro ya taarifa ya Mpito wenye haki au mpito tu – Kuwatetea wanawake walio katika sekta ya Kawi

Mifano ya kurasa zilizotumiwa

Muhtasari

Kufuatia kuzinduliwa kwa ripoti ya “Mpito Wenye Haki Au Mpito tu – Kuwatetea Wanawake Walio Katika Sekta ya Kawi, ambayoo inachunguza kuhusishwa na kuwakilishwa kwa wanawake katika nyanja muhimu za sekta ya kawi, RES4Africa inalenga kuonyesha vipengele muhimu vya matokeo ya ripoti hiyo kupitia michoro ya taarifa inayovutia sana. Vielelezo hivyo vinasistiza jinsi  RES4Africa inavyoendeleza kuhusishwa na kuwakilishwa kwa wanawake katika sekta hiyo na inatilia mkazo hitaji kuu la kuwa na wanawake wengi na wasichana katika elimu ya STEM ili kusukuma mbele mpito wa kawi wa Afrika.

Ulimwengu unapokaribia mwaka wa 2050, inakadiriwa wanawake watakuwa sehemu muhimu ya wafanyakazi wa sekta ya kawi, kwa hivyo kuandaa ujuzi na umahiri wao ni muhimu sana katika kufanikiwa kuendesha mpito wa kawi. Kupitia uwasilishaji wa michoro ya taarifa,  RES4Africa inataka kuwahimiza wanawake na washika dau katika sekta ya kawi watetee ufikiaji na usimamiaji sawa wa bidhaa na huduma endelezi za kawi.

Mchango wetu

Ubunifu
Ubunifu wa michoro
Kutayarisha michoro ya taarifa kutoka kwa ripoti ya wanawake katika kawi

Uchapishaji
Faili ya PDF ya kuwasilishwa mtandaoni

Mwaka wa uchapishaji: 2024

Lengo la Malengo ya Maendeleo Endelevu linalohusiana na chapisho