Viumbe Hai vya Misitu: Ukadiriaji wa Mazingira ya Sera ya Misitu Nchini Kenya

Mifano ya kurasa zilizotumiwa

Muhtasari

Sera ya misitu ya Kenya kihistoria imeweka kipaumbele kwa upandaji miti ndani ya misitu, mara nyingi hilo limefanyika kwa kupuuza uhifadhi wa viumbe hai. Ingawa juhudi za uhifadhi wa misitu asili zilianza katika miaka ya  1980, na kukawa na mipango maalum kama vile Mradi wa Uhifadhi wa Misitu Asili wa Kenya (KIFCON) katika miaka ya 1990, ukusanyaji data ya viumbe hai bado ni kiasi kidogo kabisa. Marekebisho chini ya Sheria ya Misitu ya 2005 (iliyorekebishwa 2016) yalitaka kuimarisha uhifadhi wa viumbe hai lakini bado hayajatekelezwa kwa njia inayofaa. Ripoti hii inaangazia jukumu la washika dau mbalimbali katika kusimamia na kuhifadhi mifumo ya ikolojia ya misitu. Inachunguza vile jamii zinazoishi karibu na misitu, kupitia Mashirika ya Misitu ya Jamii, zinaendelea kuweka kipaumbele kwa mashamba yanayoleta mapato na chakula na kupuuza viumbe hai. Inafafanua ushirikiano ulio dhaifu kati ya washika dau kama vile Huduma ya Misitu ya Kenya na Shirika la Rasilimali za Maji na jinsi kutotumia vilivyo data ya kibiografia kwa minajili ya ufuatiliaji kunazidi kulitatiza suala hilo. Ripoti hii inapendekeza kuziba pengo katika kurekodi viumbe hai vya misitu na usimamiaji, hasa kutokana na mtazamo wa kupanga taratibu na kubadilisha mtazamo.

Mchango wetu

Kuhariri
Uhariri thabiti
Kusahihisha

Ubunifu
Ubunifu wa michoro
Grafu
Uchapishaji kupitia tarakilishi

Uchapishji

PDF Iliyo tayari kuchapishwa
Faili ndogo ya PDF iliyo rahisi kushiriki na watu mtandaoni
Nakala zilizochapishwa

Mwaka wa uchapishaji: 2025

Lengo la Malengo ya Maendeleo Endelevu linalohusiana na chapisho