Zanzibar Tourism Satellite Account
Estimating The Contribution of Tourism to the Economy of Zanzibar
Mifano ya kurasa zilizotumiwa
Muhtasari
Tourism satelite accounts inatoa njia sahihi na bora iliyotambulika kimataifa ya kutathmini uzalishaji unaohusiana na utalii na viungo vyake kwa sekta mbali mbali.
Mchango wa kiuchumi wa utalii kwa uchumi wa Zanzibar ulipimwa kwa kuunda jedwali kumi za TSA. Kwa ujumla akaunti zilizoundwa zilichanganua nyenzo zote za utakaji wa bidhaa na huduma zinazohusiana na utalii katika uchumi huo. Kufuatilia shughuli za ugavi wa bidhaa na huduma na kutathmini namna ugavi unahusiana na shughuli nyingine za kiuchumi. Lengo kuu la mradi huu lilikuwa kutambua mchango wa moja kwa moja wa utalii wa kifedha kwa uchumi wa Zanzibar.
Lengo maalum lilikuwa kukadiria mahitaji na ugavi wa utalii, kuchunguza ubora unaongezwa na shughuli za utalii kwa uchumi, kutambua kiwango cha ajira kinachozalishwa na shughuli za utalii, kupima kiwango cha jumla cha fedha kisichobadilika kinachoundwa na sekta hio na kupima jumla ya kiwango cha matumizi ya shughuli za utalii na serikali.
Mchango wetu
Uhariri
Kuhariri kiundani
Kusoma kwa prufu
Picha
Kutafuta picha halisi za kudhihirisha shughuli mbali mbali za utalii na kiuchumi Zanzibar
Usanifu
Usanifu wa muundo
Kuunda michoro yenye ujumbe na grafu
Usanifu wa picha
Uchapishaji
Nakala zilizoundwa tayari kwa uchapaji
Nakala ndogo zilizoundwa ili kusambaza mtandaoni kwa urahisi
Nakala zilizopigwa chapa za uzinduzi Zanzibar
Mwaka wa uchapishaji: 2022