Uchapishaji unaoendeleza malengo ya maendeleo endelevu

Kama watia saini wa Mkataba wa Ulimwenguni wa Umoja wa Mataifa na wale wa malengo ya maendeleo endelevu ya wachapishaji, tunajitahidi kufanya kazi na washirika na wateja wetu kuhakikisha kuwa mahitaji yao ya kuripoti kuhusu hatua za kutimiza malengo ya maendeleo endelevu yanatimia. Hii itaruhusu washirika wa kimataifa na wale wa nyumbani kuhakikisha kuwa machapisho yao yanaingiliana na malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa na kuwa ujumbe wanaochapisha usiwe tu wa kuhimiza malengo haya ila pia kuharakisha hatua za kufanikisha malengo haya ya Umoja wa Mataifa kufikia 2030.

Malengo ya Maendeleo Endelevu ni nini?

Mradi wa Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa unaelezea mkusanyiko wa malengo 17 ya kimataifa, yaliyoundwa kama mwongozo wa kufikia mustakabali bora na endelevu kwa wote. Umoja wa Mataifa umeweka mwaka 2030 kama lengo la kufanikisha malengo haya. Kama watiasaini wa Mkataba wa Ulimwenguni wa Umoja wa Mataifa (UNGC) tangu kuanzishwa kwake, tumekuwa tayari kuelekeza mazoea yetu ya biashara kwa pamoja na juhudi za Umoja wa Mataifa katika kuendeleza mazoea ya biashara yanayochochea uendelevu.

Mkataba wa Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Wachapishaji

Sisi pia ni watia saini wa Mkataba wa Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Wachapishaji wa Umoja wa Mataifa. Kama wachapishaji ni jukumu letu kuhakikisha kuwa ushawishi na ufikiaji wetu unatumiwa kwa manufaa ya binadamu. Mkataba wa Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Wachapishaji wa Umoja wa Mataifa unawakilisha kujitolea kwa pamoja kufanya kazi kuelekea kujenga maisha mazuri ya baadaye katika viwanda vya uchapishaji vyote. Mkataba huu unanalenga kuimiza wachapishaji kufuata fungu fulani la maadili kwa kuchukua hatua kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu katika kipindi cha muongo wa hatua (2020 na 2030).

Malengo ya Maendeleo Endelevu kwa wote

Namna Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Wachapishaji hukusudia kuleta mabadiliko

Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa ya Wachapishaji yametoa seti ya malengo kwa wale waliopewa jukumu la kuunda ujumbe ambao malengo yao hulingana na yale ya Umoja wa Mataifa. Mkataba huu unajitahidi kuhakikisha kuwa watia saini watafanya kazi kwa kuchukua hatua zitakazochangia kutekeleza azma ya kupitisha Malengo ya Maendeleo Endelevu haya, ili kuunda kiwanda kinachofuata hatua za kimsingi za kukuza ulimwengu bora. Mkataba huu unachochea kujitolea baina ya wachapishaji kuendeleza uchapishi wa ujumbe unaohimiza usawa na uendelevu na kupitisha mazoea yana athari ndogo kwa mazingira, pia kushirikiana na kufunza washikadau katika kiwanda hicho.

Athari ya wachapishaji kwa maisha ya binadamu

Umuhimu na jukumu la wachapishaji kwa jamii ya ulimwengu haliwezi kupuuzwa. Kama waanzilishi na wapeanaji wa ujumbe wa kimaandishi, miungano ya uchapishaji ina nguvu za kuelekeza ujumbe wa kilimwengu na kufahamisha dunia na jamii ya kimataifa kwa ujumla. Ni jukumu lao kuhakikisha kuwa ujumbe unachapishwa kwa njia endelevu na yenye maadili. Hili lina uzito hata zaidi katika nchi zinazokuwa, ambako watu wengi wanategemea ujumbe uliochapishwa na wala sio ule wa mitandaoni. Kuanzia vitabu na majarida hadi mabango na vipeperushi ujumbe unaendeleza kufikiria kwetu na kufahamisha mawazo yetu.

Malengo ya Maendeleo Endelevu mahususi tunayoangazia

Kwa muktadha wetu lengo la Malengo ya Maendeleo Endelevu la nne linamaanisha kufanya kazi na wateja wetu kuhakikisha kuwa ujumbe wao wa maandishi unawasiliana kwa njia ya ufupi na wazi, ambayo inaweza eleweka kwa urahisi inapotumiwa na hadhira lengwa.

Lengo la Maendeleo Endelevu la kumi na saba linalohusu ushirikiano kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu, imaanisha tushirikiane na miungano na taasisi ambazo kazi zao huendeleza athari pana za kijamii.

Mawasiliano kuhusu maendeleo

  • Hii ni ripoti ya kila mwaka inayodhihirisha kujitolea kwetu kwa Mkataba wa Ulimwenguni wa Umoja wa Mataifa (UNGC). Kupitia kwa ripoti hii tunaweza kuwasilisha hatua tulizopiga katika kutekeleza mihimili ya Mkataba wa Ulimwenguni wa Umoja wa Mataifa kama mojawapo ya uendelevu wa shirika na wajibu wetu kwa washikadau wetu.

  • Mihimili hii inajikita katika nguzo ya haki za kibinadamu, utendaji kazi, mazingira na kupambana na ufisadi na kuongoza shughuli zetu, sera zetu na mikakati yetu katika mwaka wetu mzima wa fedha.

  • Mkataba wa Ulimwenguni wa Umoja wa Mataifa umeorodhesha mihimili kumi ambayo inawapa motisha watia saini kutumia sera endelevu zinazokusudia kumaliza ufisadi, kuhimiza haki za binadamu, kuangazia mazingira mazuri ya kikazi, na kulinda mazingira ya kibiashara.

  • Hata hivyo, malengo haya hayawezi kutimizwa bila kuwepo na kuripoti sahihi kwa mambo yanayowezekana. Kuripoti huku kunaruhusu Umoja wa Mataifa kuchunguza na kukagua maendeleo ya miungano katika kufanikisha malengo haya kufikia mwaka wa 2030 huku kwa kujumuisha mikakati ili kuongoza ufanikishaji wao au kuwachukulia hatua watiasaini wasiofuata kubaliano.

Je, ungependa kupokea mawasiliano yetu yatakayofuata ya maendeleo?

Kuwa wa kwanza kupokea mawasiliano yetu yatakayofuata ya maendeleo

© 2024 Epsilon Publishers Limited