Winnie Arwa
Mkuu wa Uendeshaji Shughuli
Winnie ni kiongozi wetu wa shughuli za uendeshaji, ambaye amepewa jukumu la kutekeleza na kuripoti kuhusu michakato na viwango vinavyofaa katika kazi zote za shirika: kuunda na kutekeleza sera ili kusaidia kufikia malengo ya kimkakati, na kusimamia shughuli za biashara ili kutimiza matarajio ya wafanyakazi na wateja. Pia anasimamia mahusiano na wauzaji, wateja, na wadau wengine. Winnie pia anasimamia utekelezaji wa taratibu zote kama usimamizi wa data, leseni za biashara,kuwajibika na viwango vya usalama.
Msingi wa Winnie upoo katika mawasiliano na uhusiano wa umma, na ana uzoefu mkubwa katika mahitaji ya mawasiliano ya kibinafsi na ya shirika. Aidha, ana uzoefu wa zaidi ya miaka mitano katika uongozi wa timu, akiwa amefanya kazi katika uongozi na maendeleo ya wafanyakazi, na kuhakikisha kuwa mahitaji ya wateja yanakidhiwa. Ana ujuzi mkubwa wa kipekee wa mipango na ujuzi wa shirika, ambao ameendeleza kwa zaidi ya miaka nane akiwa kama msimamizi.
Ana diploma katika Mawasiliano ya Umma na matangazo akizamia Mahusiano ya umma kutoka Chuo Kikuu cha Multimedia, na Shahada ya Sayansi katika Mawasiliano na Uhusiano wa Umma kutoka Chuo Kikuu cha Moi.
Winnie ana hamu ya kusoma kwa ajili ya kujifunza, kujisahihisha na kujifunza upya, na ukulima mdogo kama njia za maendeleo ya kibinafsi.